Timu za Taifa za Burkina Faso na Mali zinachuana leo katika mchezo wa kuwania tiketi ya kutinga robo fainali ya michuano ya Afcon 2023
Nyota wawili wa Yanga Stephane Aziz Ki na Djigui Diarra wanakutana katika mchezo utakaopigwa saa 2 usiku
Ni mchezo ambao baada ya dakika 90 au 120 itafahamika nani atarejea nyumbani kuungana na Yanga mapema na nani ataendelea kubaki Ivory Coast kushiriki robo fainali ya michuano hiyo
Mpaka sasa Nigeria, Angola, DR Congo, Guinea, Cape Verde na Ivory Coast tayari zimetinga robo faibali
Burkina Faso/Mali na Morocco/Afrika Kusini zinakamilisha mechi za hatua ya 16 bora leo kupata washindi wawili watakaokamilisha timu nane zilizofuzu robo fainali
Kila la kheri Diarra, kila la kheri Aziz Ki..
ADVERTISE HERE