Jana Yanga ilimtambulisha rasmi mshambuliaji mpya Joseph Guede raia wa Ivory Coast aliyesajiliwa dirisha dogo akitokea klabu ya Tuziaspor ya Uturuki
Ulikuwa utambulisho wa aina yeka ulifanyika uwanja wa Azam Complex wakati wa mapumziko katika mchezo wa kombe la FA kati ya Yanga dhidi ya Housung Fc
Guede alikaa jukwaani na mashabiki na kushuhudia kipindi chote cha kwanza pasipo wengi kumfahamu na ilipofika mapumziko ndipo taa zikazimwa, akainuliwa jukwaani na kushuka uwanjani kwa ajili ya utambulisho
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi alichagua kutomtumia katika mchezo dhidi ya Housung licha ya kuwa amefanya mazoezi kwa takribani siku nne
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema Guede ataongeza ubora na ufanisi katika safu ya ushambuliaji
Pengine Wananchi watamshuhudia Ijumaa katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa uwanja wa Kaitaba
