Matchday : Kagera Sugar vs Yanga, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Feb 2024
Matchday : Kagera Sugar vs Yanga, NBC PL

Baada ya mapumziko ya zaidi ya mwezi mmoja, ligi kuu ya NBC inarejea leo ambapo mabingwa wa ligi hiyo Yanga ni miongoni mwa timu zitakazoshuka dimbani

Yanga iko mkoani Kagera kuchuana na Kagera Sugar katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Kaitaba, muda wa mchezo ni saa 10 jioni

Kikosi cha Yanga kilitua Bukoba mapema jana na jioni vijana wa Miguel Gamondi wakafanya mazoezi yao ya mwisho katika dimba la Kaitaba

Mara nyingi mechi ya kwanza baada ya mapumziko ya muda mrefu huwa si nyepesi kwa kuwa wachezaji ndio wanarudi mchezoni

Gamondi amesema timu yake itaingia na mfumo wake wa siku zote na lengo ni kupata ushindi

Yanga ilipata mapokezi makubwa jana na bila shaka dimba la Kaitaba litapambwa kwa rangi za njano, kijani na nyeusi licha ya Yanga kuwa ugenini

Ushindi kwa Yanga utawarudisha kileleni mwa msimamo wa ligi na pengine huo utakuwa mwanzo wa safari ya kutetea ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo

Katika mchezo huo Yanga itakosa huduma ya nahodha Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Bacca ambao wamerejea kutoka Ivory Coast wakiwa majeruhi

Winga Augustine Okrah pia bado hajaimarika sawasawa kutokana na majeraha aliyopata katika michuano ya kombe la Mapinduzi

Djigui Diarra bado yuko Ivory Coast akisubiri robo fainali Afcon 2023 wakati Stephane Aziz Ki akitarajiwa kurejea nchini baada ya Burkina Faso kuondoshwa Afcon

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
16h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’