Jana Mali iliondoshwa katika michuano ya Afcon 2023 kwa kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa wenyeji Ivory Coast katika mchezo wa robo fainali
Pengine Mali watajilaumu wenyewe kwa kukosa ushindi katika mchezo ambao walitawala huku wapinzani wao wakicheza zaidi ya dakika 70 wakiwa pungufu
Mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra alikuwa langoni katika mchezo huo ambao ulikuwa wa tano kudaka huko Ivory Coast
Diarra amecheza dakika zote akiruhusu mabao manne ambapo mabao mawili aliruhusu katika mechi nne zilizopita na jana akaruhusu mengine mawili
Sasa Diarra anarejea Tanzania kuungana na kikosi cha Yanga kuendeleza mapambano ya kutetea ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo
ADVERTISE HERE