Yanga ijiandae kukabiliana na wapoteza muda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Feb 2024
Yanga ijiandae kukabiliana na wapoteza muda

Wakati Yanga inapigwa mabao 2-1 na Ihefu Fc, kulikuwa na matukio mengi ya kupoteza muda kutoka kwa wenyeji

Unaweza kusema kwa wastani mchezo ule ulipigwa dakika 60 tu, hata muda wa nyongeza haukuchezwa ipasavyo kwani matukio hayo yaliendelea

Mkoani Kagera mbinu hizo zikajirudia kwa Kagera Sugar na wakafanikiwa kupata alama moja

Jana katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji Yanga ikalazimika kusubiri mpaka dakika ya 86 kufunga bao pekee la ushindi katika mchezo ambao muda mwingi ulipotea kwa wachezaji wa Dodoma Jiji kufanya matukio yaleyale

Ujumbe ambao Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi anahitaji kuondoka nao ni kuwa atarajie kila mechi wapinzani wake watatumia mbinu hiyo kwani wanaona ndio njia pekee ya kuizuia Yanga

Lakini mbinu hii haitafanya kazi kama Yanga itakuwa ikifunga mapema. Mkakati ni kuhakikisha vijana wake wanapachika mabao ya mapema ili kuvuruga mipango ya wapinzani

Zile tano tano walizopigwa baadhi ya timu zilitokea baada ya kuwa Yanga imetangulia kufunga mapema na katika mechi ambazo huchelewa kufunga, mambo huwa magumu kadiri mechi inavyoelekea ukingoni kwa sababu matukio ya kupoteza muda huongezeka

Upande wa Bodi ya Ligi na Kamati ya Waamuzi nao wanapaswa kuja na mkakati wa kukomesha mbinu hizi zinazowanyima mashabiki burudani ya soka

Mashabiki wanalipa viingilio kutazama burudani na sio kushuhudia wachezaji wakijiangusha kila mara kama wagonjwa

Waamuzi ni lazima waongeze ukali kwa kutoa adhabu na hata muda unaoongezwa baada ya dakika 90 lazima uakisi muda uliopotea

Haiwezekani mechi iliyopotezwa dakika 15 kuongeza dakika 5 tu na pengine katika hizo dakika za nyongeza zikachezwa mbili tu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’