Mikiki mikiki ya Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambao Wananchi Yanga watashuka uwanja wa Azam Complex kuikabili Mashujaa Fc katika mchezo mwingine wa kiporo
Ni mchezo mwingine muhimu kwa Yanga kuzisaka alama tatu ili kuzidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi
Huenda baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi Ibrahim Bacca, nahodha Bakari Mwamnyeto na Augustine Okrah wakarejea leo huku kukiwa na taarifa ya urejeo wa mlinda lango Djigui Diarra
Licha ya kutofurahishwa na mbinu za wapinzani wake, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema ni lazima wacheze kama mabingwa na kuhakikisha wanatumia vyema nafasi nyingi wanazotengeneza
Yanga ilishinda mchezo uliopita dhidi ya Dodoma Jiji kwa bao 1-0 lakini ni wazi Wananchi walistahili ushindi mnono zaidi kutokana na nafasi nyingi walizokosa
Mchezo utapigwa saa 1 usiku