Klabu ya Yanga kwa kushirikiana na Bank ya NMB leo wameziundua BLACK CARD ambayo itamuwezesha Mwanachama wa klabu ya Yanga kupata huduma mbalimbali za 'VIP'
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema Black Card yenye thamani ya Tsh Milioni 1 ni kadi ya kiwango cha juu kabisa katika mapinduzi ya soka Tanzania na itafungua mlango maalum kwa Wanachama wa Yanga kupata huduma za kipekee
"Nawapongeza sana NMB kwa hili ambalo wamefanya leo. Katika kukuza usajili wa Wanachama nadhani mwendelezo huu unaleta picha ya tofauti kabisa kwenye mapinduzi sio tu ya Yanga bali kwa soka la AFRIKA. Black Card ni kadi ya kiwango cha juu kabisa katika mapinduzi ya soka Tanzania"
"Tumefungua mlango maalumu kabisa kwa wanachama wetu kupata huduma za ziada. Hivyo Yanga tumekaa na NMB na kufungua majadiliano kuhakikisha wanapata huduma imara na madhubuti"
"Na kadi hizi zinatolewa katika matawi yote ya NMB. Thamani ya Black Card ni Tsh 1,000,000. Tumefanya utafiti maalumu kuhakikisha kadi hii inampa Mwanachama wetu thamani na huduma bora na za kisasa kuhakikisha tunamthaminisha na kumuongezea faida ya kuwa mwananchama wetu"
"Kupitia kadi hii Mwanachama atapata tiketi 10 za VIP msimu mzima (thamani ya tiketi ya VIP 30,000). Mwanachama atapata jezi seti sita za msimu mpaka jezi za watoto (thamani ya jezi 50,000). Kadi hii itamwezesha kupata punguzo la huduma ya afya katika hospital ya Aga Khan kuanzia 10% Mwanachama mwenye “black card," alisema
Nae Filbert Mponzi ambaye ni Mkurugenzi wa Biashara NMB alieleza faida ambazo Mwanachama mwenye Black Card atazipata kutoka benki hiyo
"Miongoni mwa faida ya Black Card utapata fursa ya kuingia VIP LOUNGE katika kiwanja chochote cha ndege duniani. Black Card ina bima endapo utapoteza mzigo wako safarini unalipwa dola 3000"
"Endapo mzigo wako pia utachelewa utalipwa dola 300. Ikitokea unasafiri kwa ndege ndani ya nchi au nje ya nchi ndege ikaahirisha safari unalipwa mpaka dola 7500. Muhimu ni kuhakikisha unanunua tiketi ya ndege ili uweze kunufaika na BIMA na ya namna hii"
"Ukiwa na Black Card, unaweza kupata mkopo mpaka 500,000 bila kufuata utaratibu wowote unaingia tu kwenye menyu yako au APP yako unajipekulia mkopo. Vile vile ukienda baadhi ya sehemu za kupata chakula ukalipia na black card unapata punguzo mpaka 15%," alisema