Mwamnyeto, Aziz Ki wako tayari kuikabili Prisons

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Feb 2024
Mwamnyeto, Aziz Ki wako tayari kuikabili Prisons

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wako mkoani Mbeya ambapo jioni ya leo wataadhimisha miaka 89 kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa uwanja wa Sokoine

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ameendelea kushuhudia kikosi chake kikiimarika baadhi ya wachezaji wakirejea kikosini baada ya michuano ya Afcon 2023 inayofikia tamati leo huko Ivory Coast

Wachezaji Stephane Aziz Ki na nahodha Bakari Mwamnyeto huenda wakarejea kikosini mkoani Mbeya leo

Mwamnyeto alipata majeraha wakati yuko kwenye majukumu ya Stars sasa amepona na amejumuishwa katika kikosi kilichosafiri Mbeya

Aziz Ki alichelewa kurudi kutokana na kuuguliwa na mzazi wake lakini nae yuko tayari na pengine leo atakuwa na dakika zake mkoani Mbeya

Beki Ibrahim Bacca yeye alirejea kikosini mchezo uliopita dhidi ya Mashujaa Fc wakati Dickson Job na Mudathir Yahya wao walirejea mapema

Job ameshiriki mechi zote tatu za ligi wakati Mudathir akishiri mechi mbili na kufunga katika kila mchezo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
30m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
49m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
54m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’