Jana Yanga ilikuwa mkoani Mbeya kuikabili Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu ya NBC ambao Wananchi walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kuzidi kujiimarisha killeni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 40
Katika kikosi kilichopaswa kuanza, jina la mshambuliaji Kennedy Musonda lilikuwa miongoni mwa waliopaswa kucheza mchezo huo
Hata hivyo Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi alilazimika kufanya mabadiliko ya dharura akimtoa Musonda na nafasi yake kuanza Farid Mussa
Hii ni baada ya Musonda kubanwa na ugonjwa wa macho 'red eyes' ambayo ilimfanya kuwa na uono hafifu
"Musonda alipata changamoto ya ugonjwa wa macho. Awali tuliamini angeweza kumuda mchezo lakini muda mfupi kabla ya mechi tukabaini hali hiyo ingemsumbua"
"Nafurahi anaendelea vizuri na pengine atakuwa sawa katika mchezo unaofuata (dhidi ya KMC)," alisema Gamondi
Yanga ilirejea Dar es salaam kutokea Mbeya mapema leo ambapo Wananchi watakuwa na siku tatu za kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya KMC