Takwimu za Gamondi ligi kuu ni zaidi ya Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Feb 2024
Takwimu za Gamondi ligi kuu ni zaidi ya Nabi

Yanga imekamilisha mechi 15 za duru ya kwanza ligi kuu ya NBC 2023/24 ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi na alama 40

Kwa mujibu wa takwimu, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amefanya vizuri zaidi katika mechi 15 za kwanza msimu huu kuliko ilivyokuwa msimu uliopita wakati Yanga ikinolewa na Nasreddine Nabi

Katika msimu wa 2022/23, Yanga ilimaliza duru ya kwanza ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 38 ambazo ni alama mbili pungufu ya alizokusanya Gamondi msimu huu

Aidha katika msimu huo Yanga ilipachika mabao 28 na kuruhusu mabao nane wakati kikosi cha Gamondi msimu huu kimepachika mabao 36 na kuruhusu mabao nane pia

Msimu huu Yanga imefunga mabao nane zaidi kulinganisha na mabao waliyofunga msimu uliopita baada ya mechi 15

Itoshe kusema Gamondi ameanza vyema majukumu yake na matarajio ya Wananchi ni kuipa Yanga mataji zaidi kama alivyofanya mtangulizi wake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’