Baada Afcon 2023 kufika tamati huko Ivory Coast, michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika inarejea Ijumaa ya wiki hii kwa mchezo mmoja wa kiporo kundi D kupigwa
CR Belouizdad watakuwa wenyeji wa Al Ahly katika mchezo utakaopigwa huko Algeria
Al Ahly ndio vinara wa kundi D wakiwa na alama tano sawa na Yanga inayoshika nafasi ya pili
Matokeo ya mchezo huu yana umuhimu wa kipekee kwa Yanga inayowania nafasi ya kutinga robo fainali
Kama Al Ahly watashinda, basi Yanga itahitaji kushinda mchezo unaofuata dhidi ya CR Belouizdad wiki ijayo ili kuwa na nafasi nzuri ya kutinga robo fainali
Yanga na Belouizdad zitaumana Februari 24 katika uwanja wa Benjamin Mkapa wakati Medeama na Al Ahly zitachuana Februari 23
Hizi ni mechi za lala salama kila timu ikihitaji alama tatu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali