Wachezaji wa Yanga Kibwana Shomari na Clement Mzize wamepigwa faini ya Tsh Milioni 1 kila mmoja kufuatia matukio ya kuondosha taulo la golikipa katika mechi za ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc na Dodoma Jiji
Yanga pia imepigwa faini ya Tsh Milioni 1 kwa kosa la mashabiki kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons
Faini nyingine ya Tsh Milioni 1 kwa kosa la kuchelewa kurejea uwanjani kwenye kipindi cha pili katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji
Aidha mchezaji wa Tanzania Prisons Jeremiah Juma amefungiwa mechi tatu na faini ya Tsh Milioni 1 kwa kosa la kumkanyaga Yao Kouassi





ADVERTISE HERE