Gamondi apania ushindi dhidi ya KMC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Feb 2024
Gamondi apania ushindi dhidi ya KMC

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Gamondi amesema anatambua mchezo huo utakuwa tofauti na mchezo wa kwanza waliocheza jijini Dar es salaam lakini jambo muhimu kwao ni ushindi na kuwapa furaha mashabiki

"Nafurahi tumekuwa na wakati mzuri hapa tangu tulipowasili. Hali ya hewa ni nzuri na wachezaji wanafurahia mazingira haya"

"Mara zote huwa nasema napenda kucheza mchezo wa kuburudisha lakini naimani hautakuwa mchezo rahisi na sisi tupo hapa kwaajili ya kufanya vizuri ili kutimiza malengo yetu,” alisema

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, mlinzi wa kushoto Nickson Kibabage amesema wanatambua mechi za raundi ya pili sio nyepesi lakini watapambana ili kuhakikisha wanashinda ili kutimiza malengo

"Raundi ya pili huwa ni ngumu lakini kwa ukubwa wa klabu ya Yanga tunahitaji kushinda kila mechi, sisi wachezaji kila sehemu tunayokwenda huwa tunatambua umuhimu wa mechi na tunaamimi kwenye kuwapa furaha mashabiki wetu," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’