Fainali yetu ni dhidi ya CR Belouizdad - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Feb 2024
Fainali yetu ni dhidi ya CR Belouizdad - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki na wanachama wa timu hiyo kukaa tayari kwa mchezo wa kuwania kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya CR Belouizdad

Jumamosi ijayo, Februari 24 Yanga itakuwa mwenyeji wa Belouizdad katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Jana Belouizdad ilichuana na Al Ahly katika mchezo wa kiporo uliomalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana

Matokeo hayo yamefanya Yanga na Belouizdad zilingane zote zikiwa na alama tano Belouizdad wakikaa nafasi ya pili kwa faida ya mabao

Al Ahly wanaongoza kundi D wakiwa na alama sita wakati Medeama wanashika mkia wakiwa na alama nne. imahesabu timu zote zina nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali

"Kundi la Kiume, nafasi bado iko wazi kwa kila Timu. Sisi Yanga fainali yetu ni uwanja wa Mkapa Vs Belouzidad, tarehe 24/2/202"

"Mpango wetu ni robo fainali. Na Tutautimiza mpango huu kama Tutaungana pamoja na kwenda uwanjani kuwapa nguvu wachezaji wetu siku hiyo"

"Uwanja kujaa ndio silaha yetu ya kwanza ya kumpunguza makali Mwarabu.. Inawezekana Wananchi .. ROBO FAINALI INATUSUBIRI," alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’