Yanga imetakata uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Mudathir Yahya ameendeleza kasi yake ya kuzifumania nyavu leo akifunga mabao mawili moja likiwa la mapema dakika ya kwanza
Alikuwa Nickson Kibabage aliyetengeneza mabao mawili yaliyofungwa na Mudathir na Pacome Zouzoua ambaye alipigilia msumari wa mwisho
Clement Mzize atajilaumu kwa kukosa nafasi nyingi za wazi katika kipindi cha kwanza huku Joseph Guede aliyeingia kipindi cha pili nae akikosa nafasi kadhaa
Ni alama tatu muhimu kwa Yanga ambazo zinawaweka Yanga kileleni kwa tofauti ya alama saba baada ya kufikisha alama 43
ADVERTISE HERE