Yanga vs CR Belouizdad ni mechi ya kisasi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Feb 2024
Yanga vs CR Belouizdad ni mechi ya kisasi

Baada ya ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa mkoani Morogoro jana, Wananchi sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Ni Jumamosi ya Februari 24, Yanga itakuwa mwenyeji wa CR Belouizdad katika mchezo wa raundi ya tano kundi D utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa saa 1 usiku

Hii ni kama fainali kwa Yanga kwani Wananchi wanahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali

Yanga itaingia katika mchezo huu ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza ulioipigwa Algeria

Hivyo hii ni mechi ya kisasi, deni inapaswa lilipwe mbele ya mashabiki 60,000 ambao wanatarajiwa kujitokeza kuishangilia Yanga

Aidha ushindi wa zaidi ya mabao 3 unaweza kutosha kuipeleka Yanga robo fainali hasa kama itatokea Medeama watakosa ushindi dhidi ya Al Ahly katika mchezo utakaopigwa Februari 23 huko Ghana

Katika msimamo wa kundi D, Al Ahly wako kileleni wakiwa na alama sita, Belouizdad iko nafasi ya pili ikiwa na alama tano sawa na Yanga timu hizo zikitofautiana mabao

Medeama wako nafasi ya nne wakiwa na alama nne. KIla timu kundi D ina nafasi ya kwenda robo fainali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’