Mechi dhidi ya CR Belouizdad amepewa mtu kweli kweli ambaye michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu ameitendea haki
Pacome Zouzoua ndiye kinara wa mabao katika michuano hiyo akiweka kambani mabao matatu
Sankara Karamoko aliyekuwa akiitumika Asec Mimosas ndiye mchezaji pekee aliyekuwa amemzidi Pacome idadi ya mabao. Lakini Karamoko hayupo tena Asec akitimkia barani Ulaya
Hii ni mechi ya heshima kwa Yanga, ni ushindi tu ambao utaweka hai matumani ya Wananchi katika harakati za kufuzu robo fainali
Pacome hakuwaangusha Wananchi katka mechi zote nne za hatua ya makundi
Alifunga bao lililoipa Yanga alama moja katika mchezo dhidi ya Al Ahly katika dakika za lala salama muda ambao Wananchi walikuwa wamepoteza matumaini
Akafunga bao pekee kule Ghana kuirejesha Yanga mchezoni dhidi ya Medeama, Wananchi wakarejea nyumbani na alama moja
Katika mchezo wa pili dhidi ya Medeama uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga ilihitaji ushindi
Ni Pacome aliyefungua kurasa ya mabao ya Yanga kabla ya Kennedy Musonda na Mudathir Yahya kuongeza mawili na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0
Bila shaka Pacome Day itafana kwa mashabiki wa Yanga kumuonyesha fundi huyu wa ni kwa kiasi gani wanathamini mchango wake