Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi kikosi chake kimeweka rekodi ya aina yake katika michuano mbalimbali msimu huu
Kwa makocha wapya, mara nyingi misimu yao ya kwanza huanza na changamoto nyingi, lakini hali ni tofauti kwa Gamondi
Katika msimu huu mpaka sasa mashabiki wa Yanga wameshuhudia vipigo vikubwa vikitolewa na timu yao pengine kuliko wakati mwingin wowote
Yanga imeshinda mechi saba kwa ushindi wa mabao matano, hii ni rekodi kwa Wananchi kufunga mabao 35 katika mechi saba
KMC walikuwa wa kwanza kukumbana na 5G ya Yanga pale Azam Complex wakafuatiwa na Asas Fc ambao nao wakawapisha JKT Tanzania
Hii 5G ilikuwa ni lazima kila mmoja aonje ndio maana Simba nao wakaikimbilia pale uwanja wa Benjamin Mkapa Novemba 05 2023
Mwezi Januari 2024 Wananchi wakaelekea visiwani Zanzibar nako wakagawa 5G kwa Jamhuri
Vipigo hivyo vikaendelea katika michuano ya kombe la FA, Housung wakapewa zawadi yao na jana Polisi Tanzania nao wakakabidhiwa 5G yao
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametahadharisha kuwa muda sio mrefu dozi hii itaongezeka baada ya kuona kuna wengi wanaoihitaji!