Yanga imejihakikishia kuvuna Dola 900,000 (zaidi ya Sh2.3 bilioni) kwa kutinga robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika
Mabingwa hao wa Tanzania Bara wamefuzu hatua hiyo baada ya juzi kuichapa CR Belouizdad mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam
Wananchi walisubiri miaka 25 kutinga hatua ya makundi na sasa wanafurahia mafanikio makubwa zaidi
Mkakati wa Yanga sasa ni kuvuka robo fainali na pengine kuweka rekodi ya kipekee katika mashindana ya CAF msimu huu
Kama Yanga itafanikiwa kutinga nusu fainali basi dau litaongezeka hadi kufikia Sh3.1 bilioni huku ikifanikiwa kutinga fainali itavuna Sh5.1 bilioni . Kama itaibuka na ubingwa itavuna zaidi ya Sh10.2 bilioni
ADVERTISE HERE