Paqueta alia na Pacome, Aziz Ki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Feb 2024
Paqueta alia na Pacome, Aziz Ki

Kocha Mkuu wa CR Belouizdad Marcos Paqueta amekiri kuwa mpango wake wa mechi dhidi ya Yanga ulivurugwa na ubora waliokuwa nao nyota wa Yanga katika mchezo wa ligi ya mabingwa uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa juzi na kuishuhudia Yanga ikitinga robo fainali baada ya ushindi wa mabao 4-0

Baada ya kushinda mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Algeria, CR Belouizdad walitua Tanzania wakiwa na matumaini makubwa lakini hawakuamini kilichotokea dimba la Mkapa wakitoka vichwa chini na vilio baada ya kipigo cha 'mbwa mwizi'

Akizungumza baada ya mchezo huo, Paqueta alisema licha ya kuwa na mkakati maalum wa kukabiliana na Yanga katika mchezo huo, hata hivyo mpango huo haukufanikiwa kutokana na ubora na uwezo binafsi wa baadhi ya nyota wa Yanga akiwataja Pacome Zouzoua na Stephane Aziz Ki

"Yule mwenye jezi namba 26 (Pacome) ndiye alitupa wakati mgumu kwenye mchezo huu, alitusumbua sana licha ya kwamba tulishajipanga kuhakikisha hafanyi kazi kwa utulivu"

"Alikuwa na makali kila alipogusa mpira kuelekea lango letu, ana akili na kasi, kwangu Mimi tulifanya makosa kutomdhibiti vyema".

"Aliyevaa jezi namba 10 pia (Azizi Ki) alikuwa na mchezo mzuri, alikuwa na pasi za hatari kwenda kwenye eneo letu la ulinzi, tulifanya makosa mengi yaliyotugharimu," alisema Paquet raia wa Brazil

Licha ya kutofunga bao katika mchezo huo Pacome aliitendea haki siku hiyo iliyopewa jina lake 'Pacome Day'

Alihusika katika mabao mawili akitoa pasi kwa Joyce Lomalisa ambaye krosi yake ilimaliziwa na Mudathir Yahya pia akitoa pasi ya bao la tatu lililofungwa na Kennedy Musonda

Aziz Ki alifunga bao la pili na kutoa pasi ya bao la nne lililofungwa na Joseph Guede

Lakini pia alitoa pasi adimu kwa Pacome ambaye hakufanikiwa kufunga huku pia Pacome nae akimtengenezea Aziz nafasi nyingine ambayo alishindwa kuitumia

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’