Wananchi wana kila sababu ya kujivunia mafanikio ya klabu yao katika michuano ya CAF CC na CAF CL katika misimu hii miwili
Baada ya Yanga kutinga robo fainali ya ligi ya mabingwa imepanda mpaka nafasi ya 11 katika viwango vya CAF kwa kuzingatia mafanikio ya miaka mitano
Ni hivi; Yanga imehitaji miaka miwili tu kukusanya alama 31, na kupanda juu ya viwano kutoka nafasi ya 75 (2021/22) mpaka nafasi ya 11
Bado Yanga ina nafasi ya kusogea juu zaidi kama itafanikiwa kuvuka hatua ya robo fainali kwa kutinga nusu fainali na hata fainali zaidi
Huu ni msimu wa Yanga kufyeka kile kichaka cha Kimataifa ambacho watani zao wamekuwa wakikitumia kujificha!

ADVERTISE HERE