Mashabiki wa Yanga ni wa pekee - Pacome

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Feb 2024
Mashabiki wa Yanga ni wa pekee - Pacome

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua ameeleza ni kwa jinsi gani alivyoguswa na upendo wa mashabiki wa Yanga wakati wa Pacome Day ambayo ilishuhudiwa Yanga ikitinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya CR Belouizdad

Akizungumza muda mfupi kabla kukwea pipa kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wa kukamilisha hatua ya makundi, Pacome alithibitisha kauli iliyotolewa awali na msemaji wa Yanga Ali Kamwe kuwa alicheza mechi dhidi ya CR Belouizdad akiwa majeraha

Pacome alibainisha kuwa upendo na hamasa aliyoipata kutoka kwa mashabiki ilimfanya ajihisi ana deni kubwa na kuwa tayari kuhatarisha maisha yake ya soka

"Ni kweli niliumia siku moja kabla ya mchezo dhidi ya CR Belouizdad ulikua wakati mgumu sana kwangu nakumbuka wachezaji wenzangu wote walikua tayari kwa mchezo"

"Ilivyofika asubuhi niliufuata uongozi wa Yanga pamoja na kocha nikamwambia sidhani kama ni sahihi kwangu kukaa kwa kubweteka nimeona ni kwa namna gani mashabiki wamejiandaa kwaajili ya hii siku yangu iweje leo hii na mimi nishindwe kufanya jambo kwaajili yao?"

"Namshkuru Mungu alikua upande wangu na Yanga kwa ujumla tukafanikiwa kuifunga CR Belouzidad goli 4 ambazo zilituvusha moja kwa moja"

"Pengine najivunia kuingia katika historia hii kubwa ya klabu kubwa kama Yanga kuwa miongoni mwa wachezaji walioisaidia timu yao kutinga hatua ya makundi baada ya miaka 25 pamoja na kutinga hatua ya robo fainali kwa mara ya Kwanza"

"Tunaelekea Misri tukiwa tunauhitaji sana mchezo pamoja na nafasi ya kwanza wananchi waongeze dua kwasababu ni watu wenye upendo sana na wachezaji wao naimani itatusaidia sana," alisema Pacome

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’