Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema Al Ahly ni moja ya timu anazozipa nafasi ya kucheza fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu
Hersi jana alialikwa na kufanya mahojiano maalum na Al Ahly TV ambapo pamoja na kuitaja Al Ahly, Hersi pia aliitaja Mamelodi Sundowns kuwa na nafasi ya kufika fainali
"Binafsi naamini fainali ya CAF msimu huu ni Al Ahly na Mamelodi Sundowns. Al Ahly na Mamelodi ni timu zenye mikakati na ubora wa hali ya juu kwa sasa Barani Afrika"
"Ikumbukwe Al Ahly ndio timu yenye uwekezaji mkubwa tena inapofika hatua za mtoano katika michuano hii, huku Mamelodi wakiwa ni mabingwa AFL na sidhani itakuwa rahisi kwao kuishia robo au nusu fainali," alisema Hersi
Kwa wale 'waliosoma Cuba' wanaelewa lengo la Injinia Hersi ni kuiondolea presha Yanga ambayo kesho itachuana na Al Ahly hapo Misri
Kama angeitaja Yanga katika orodha ya klabu anazoamini zitacheza fainali, ni kama angewapa Al Ahly ramani ya vita, jambo muhimu wanapaswa kuendelea kuamini Yanga haina malengo makubwa katika michuano hiyo
Msimu huu Yanga iliweka malengo ya kuingia hatua ya makundi lakini sasa iko robo fainali. Ilikuwa hivyo msimu uliopita katika michuano ya kombe la Shirikisho (CAF CC), iliweka malengo ya makundi na ikacheza fainali