Zikiwa zimebakia saa chache kabla ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara hawajakutana na Welayta Dicha FC kutoka Ethiopia, Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, amesema kuwa kutowaruhusu wapinzani wao kupata bao lolote hapa nyumbani ni moja ya mipango waliyoiandaa.
Yanga itawakaribisha Welayta Dicha FC katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano wa mashindano ya Kombe la Shirikisho Africa utakaofanyika kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Nsajigwa amesema mbali na kusaka mabao ya mapema, kuruhusu mpinzani kukufunga nyumbani kwenye mashindano hayo ya kimataifa ni sawa na kujiweka "njia panda".
Amesema kuwa nguvu ya kusaka mabao inatakiwa ilingane na ile ya kuzuia mpinzani asipate bao na endapo wakifanikiwa kutimiza malengo hayo, anaamini kikosi chake kitakuwa kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele katika mashindano hayo yanayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika
"Moja ya mambo ambayo tunatakiwa kuhakikisha tunafanya hapa nyumbani ni kutokubali kufungwa, hata kama ni bao moja, haitakiwi, tunahitaji kuwa na nguvu sawa kwenye safu ya ushambuliaji na safu ya ulinzi, tunawakumbusha kuwa makosa ya kwenye ligi tusiyarudie," alisema beki huyo wa zamani wa Yanga.
Nipashe

ADVERTISE HERE