Mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra anashika nafasi ya tatu miongoni mwa magolikipa wenye 'cleensheet' nyingi msimu huu
Diara aliyetwaa tuzo ya mlinda lango bora wa ligi kuu kwa misimu miwili mfululizo, msimu huu amekusanya cleensheet 6 akiwa nyuma ya Vumiley Matampi (9) na John Noble (7)
Ni suala la muda kwa Diarra kurudi kileleni eneo alilotawala tangu alipotua Yanga misimu miwili iliyopita
Diarra alikosa takribani mechi tano kutokana na majukumu ya timu ya Taifa ya Mali katika michuano ya Afcon 2023 iliyofanyika Ivory Coast mwezi uliopita

ADVERTISE HERE