Tangu alipojiunga na Yanga, kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua alijipambanua kwa umahiri wake uwanjani
Tofauti ya Pacome na wachezaji wengi baadhi yao wanaotamba hapa nchini, ni kuwa yeye sio mchezaji wa mechi moja
Pacome atauwasha akicheza dhidi ya Housung Fc ya Njombe lakini pia atauwasha akicheza dhidi ya Al Ahly
Ndio maana amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa msimu huu
Katika mechi sita za Ligi ya mabingwa, Pacome amefunga mabao matatu na kutoa pasi mbili za mabao. Huku kwenye ligi kuu ana mabao sita na pasi nne za mabao
Kiufupi, Pacome amejipambanua kwa kazi yake uwanjani, hahitaji kupigiwa debe huko mitandaoni
Hii mijadala inayoanzishwa kumfananisha na wachezaji wengine nafikiri ni kumkosea heshima kwa sababu Pacome ni Pacome na hao wengine ni wao
Hakuna mwananchi mwenye mashaka na ubora wa Pacome kwani tayari amedhihirisha
Wale wanaomfananisha na wachezaji wao wamsubiri uwanjani tena katika mechi ya pili kwenye ligi baada ya ile ya kwanza kuwa sehemu ya kikosi kilichogawa dozi ya 5G na hao wachezaji wao wakiwemo