Musonda wa CAF ni hatari

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Mar 2024
Musonda wa CAF ni hatari

Yawezekana kwenye ligi kuu ya NBC haonekani kuwa na ufanisi mzuri mbele ya lango, lakini Kennedy Musonda amejipambanua kuwa mchezaji muhimu wa Yanga katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu

Katika kampeni ya michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu huu kuanzia hatua ya awali, Musonda amehusika katika mabao sita akifunga manne na kutoa pasi mbili za mabao

Katika hatua za awali alifunga mabao mawili dhidi ya Asas Fc na El Merrikh wakati kwenye makundi amefunga mabao mawili katika mechi dhidi ya Medeama na CR Belouizdad huku pia akitoa assist mbili katika mechi hizo

Hata msimu uliopita katika michuano ya kombe la Shirikisho, Musonda alikuwa na mchango mkubwa akishirikiana vyema na Fiston Mayele

Nyota huyo kutoka Zambia alihusika katika mabao sita, akifunga matatu na kutoa pasi tatu za mabao

Haishangazi kuona Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi akimjumuisha Musonda katika kikosi chake kwenye mechi muhimu za kuhitaji ushindi na hajamuangusha

Bila shaka Wananchi watarajie kumuona Musonda akihitimisha msimu kibabe zaidi katika duru hili la pili ndani ya ligi kuu ya NBC

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
56m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’