Licha ya kukiri kuwa Yanga inakabiliwa na mchezo mgumu wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo Fc hapo kesho, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema timu imepata maandalizi mazuri kuelekea mchezo huo hivyo anaamini watapata matokeo mazuri
Baada ya ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa uwanja wa Azam Complex, kesho Yanga iko ugenini huko Ruangwa wakiwania alama tatu dhidi ya wenyeji wao, Namungo FC
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Gamondi alisema anatambua aina ya mchezo wanakwenda kukabiiana nao, wamejiandaa
"Tumefanya maandalizi mazuri kuelekea mchezo huo, matumaini yangu ni kuwa tunakwenda kuwa na mchezo mzuri dhidi ya Namungo hapo kesho"
"Nafahamu, mara zote timu nyingine zinapokutana na Yanga huwa zinajituma ili waoneshe ubora wao, hivyo tumejiandaa kukabiliana nao na tunahitaji ushindi," aalisema Gamondi
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, mlinda lango Metacha Mnata amesema wako tayari kwa mchezo huo wanachosubiri ni muda tu ufike
"Kwa niaba ya wachezaji wenzangu tunasubiri kesho ifike ili tuoneshe tulichojiandaa kwakuwa tuna lengo la kuwapa furaha wananchi. Hivyo nawaomba Wananchi wajitokeze kwa wingi kutusapoti ili tutimize lengo letu la kubeba alama tatu," alisema
Yanga imefanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Majaliwa tayari kwa mchezo huo Wananchi wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-0 mara ya mwisho timu hizo zilipokutana katika uwanja huo msimu uliopita