Baada ya ushindi 'mujarab' wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo Fc, kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya mchezo unaofuta
Jumatatu, March 11 Yanga itakuwa uwanja wa Azam Complex kuikabili Ihefu Fc katika mchezo nyingine kwa Wananchi kuwania alama tatu
Hii itakuwa mechi ya kisasi, Wananchi wana kumbukumbu ya matokeo ya duru ya kwanza kule Mbarali, Ihefu Fc ilishinda mabao 2-1 na kuwa timu pekee iliyoweza kuondoka na alama zote tatu dhidi ya Yanga msimu huu
Msemaji wa Yanga Ali Kamwe amesema ushindi ndio matokeo pekee ambayo Yanga inahitaji
Kamwe alitaja viingilio vya mchezo huo ambapo VIP A ni Tsh 20,000/-, VIP B ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000
Mchezo huo utapigwa saa 12 jioni...
ADVERTISE HERE