Hatimaye ile siku imewadia! Yanga na Ihefu Fc sio milima hatimaye leo wanakutana tena!
Ni katika mchezo wa ligi kuu ya NBC ambao utapigwa uwanja wa Azam Complex, saa 12 jioni
Wananchi wanasema leo ni siku ya kulipa kisasi kwa Ihefu Fc. Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana Mbarali mechi ya duru ya kwanza, Yanga ilikubali kipigo cha mabao 2-1
Ni mchezo pekee ambao Yanga wamepoteza msimu huu hivyo leo utaona ni kwa kiasi gani Wananchi leo wanataka ushindi
Habari njema kwa Yanga ni kurejea kikosini kwa baadhi ya wachezaji ambao walikosa mchezo uliopita dhidi ya Namungo Fc kutokana na sababu mbalimbali
Mlinda lango Djigui Diarra, beki wa pembeni Joyce Lomalisa, kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua na washambuliaji Kennedy Musonda na JOseph Guede wote wamerejea
Mchezaji pekee ambaye bado ataendelea kukosekana ni Khalid Aucho aliyefanyiwa upasuaji mdogo wa goti
Hata hivyo hautakuwa mchezo mwepesi kwani Ihefu Fc sio wanyonge. Timu hiyo imeimarika zaidi baada ya usajili waliofanya kwenye dirisha dogo
Ni wazi itakuwa mechi ngumu lakini Yanga ikiwa katika dimba la Azam Complex, hakuna timu iliyofanikiwa kuizuia msimu huu