Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema wako tayari kwa mchezo wa kwanza wa kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho dhidi ya Welayta Dicha kesho Jumamosi, April 07.
Akizungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa habari leo, Nsajigwa amesema kikosi cha Yanga kimemaliza salama kambi iliyowekwa mkoani Morogoro kwa siku tatu na kimerejea jijini Dar es salaam leo.
Amesema wachezaji wote waliokuwa kwenye kambi hiyo wako tayari kwa mchezo.
Nsajigwa amesema benchi la Ufundi limejipanga kikamilifu kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo huo wa kwanza unaopigwa kwenye ardhi ya nyumbani.
Amesema licha ya Dicha kuonekana kama timu ya kawaida lakini sio timu ya kubeza hivyo hawawezi kuwadharau wapinzani wao ambao waliwatoa moja ya vigogo wa Afrika, Zamaleki.
Naye Afisa habari wa Yanga Dismas Ten amesema bado CAF haijatoa majibu juu ya swala la Kelvin Yondani aliyezuiwa kucheza mchezo huo kutokana na kuwa na kadi mbili za njano.
Uongozi wa Yanga ulituma malalamiko CAF kutaka mchezaji huyo aruhusiwe kucheza kwa kuwa kwa mujibu wa takwimu walizonazo, hana kadi mbili za njano.
Hivyo Yanga italazimika kutomtumia mchezaji huyo sambamba na Obrey Chirwa, Papi Tshishimbi na Said Juma kwani hakuna uwezekano malalamiko yao yakafanyiwa kazi kesho Jumamosi kwa kuwa sio siku ya kazi.
Kuhusu washambuliaji, Donald Ngoma na Amissi Tambwe, Ten amesema wawili hao wamekuwa sehemu ya wachezaji waliokuwa wakifanya mazoezi kambini mkoani Morogoro.
Amissi Tambwe hataweza kucheza mchezo huo kwa kuwa ametonesha tena jeraha lake la goti linalomsumbua.
Kwa upande wa Ngoma, ana asilimia 50 za kucheza au kutocheza, benchi la Ufundi ndio lina uamuzi wa mwisho.

ADVERTISE HERE