Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo kwa mechi mbili kupigwa ambapo moja ya mechi hizo itawahusisha mabingwa watetezi Yanga ambao watakuwa dimba la Azam Complex kuikabili Geita Gold katika mchezo utakaopigwa saa 2:15 usiku
Yanga iko katika kiwango bora sana mchezo uliopita wakishinda mabao 5-0 dhidi ya Ihefu Fc
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema malengo ya timu yake ni kushinda mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea
Gamondi amesema pamoja na kiwango bora walichonacho sio kila mechi watafunga mabao matano, hivyo jambo muhimu kwake ni ushindi bila ya kujali watafunga mabao mangapi
Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imekusanya alama 49, ambazo ni alama tano mbele ya Azam Fc iliyo nafasi ya pili na alama saba mbele ya Simba iliyo nafasi ya tatu
