Bao alilofunga katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold jana limemrejesha Stephane Aziz Ki kileleni katika mbio za ufungaji bora akifikisha mabao 13
Aziz Ki sasa anahitaji kufunga mabao manne tu katika mechi 11 zilizosalia kuifikia rekodi ya mabao 17 ya Fiston Mayele liyofunga msimu uliopita na kuwa mfungaji bora wa ligi ya NBC akifungana na Saido Ntibazonkiza wa Simba
Huu unaweza kuwa msimu bora zaidi kwa Aziz Ki katika maisha yake ya kusakata kabumbu akiwa na uwiano mzuri wa kufunga na kutoa pasi za mabao (7)
Kituo kinachofuata ni Azam Fc, timu ambayo anapenda kuifunga, pengine katika mchezo huo utakaopigwa Jumapili kunako uwanja wa Benjamin Mkapa atazidi kuikaribia rekodi hiyo
Katika mchezo wa duru ya kwanza, Aziz Ki alifunga hat-trik na kuisaidia Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-2