Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo kwa mabingwa watetezi Yanga kushuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Azam Fc
Huu ni mchezo muhimu sana kwa Yanga katika mkakati wake wa kutetea ubingwa wake kwa msimu wa tatu mfululizo
Vita ya ubingwa ilianza na farasi watatu lakini kama Yanga itaifunga Azam Fc leo, ni wazi farasi mmoja atadondoka na huku farasi mwingine ambaye ni Yanga akijiweka katika nafasi nzuri ya ubingwa
Hii ni mechi ambayo Yanga haitakuwa ikicheza dhidi ya Azam Fc pekee, bali hata watani zao Simba watakuwa upande wa Azam wakitamani Wananchi wasiondoke na alama tatu kwani wanafahamu, ushindi kwa Yanga itakuwa ishara ya taa ya kijani kuelekea ubingwa wa 30
Baada ya mechi hii zitakuwa zimesalia mechi 10 kwa Yanga kumaliza msimu wakati upande wa Azam Fc zitakuwa zimesalia mechi 9 na kama Yanga itashinda gap la pointi dhidi ya Simba zitakuwa 10 na Azam Fc 11 huku Wananchi wakiwa na mechi moja ya kiporo na Simba mechi mbili
Katika mechi zilizokutanisha timu hizo misimu miwili iliyopita, Yanga imeshinda zote, hivyo ni wazi leo utaona kwa kiasi gani Azam Fc wataingia na ari kubwa kutaka kumaliza uteja
Kwa Yanga hii itakuwa mechi kama zilivyo nyingine na pengine Miguel Gamondi anaweza kuitumia kama kipimo cha kwanza kuelekea robo fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi
Ni saa 2:30 usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa