Leo derby ya Dar es salaam inapigwa! Ni mchezo wa ligi kuu kati ya Azam Fc dhidi ya Yanga utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa saa 2:30 usiku
Ni mchezo ambao hesabu za Wananchi ziko katika alama tatu ambazo zitawaweka katika nafasi ya kutetea ubingwa
Yanga inakwenda katika mchezo huo ikiwa na silaha zote muhimu, ni kiungo Khalid Aucho akiwa mchezaji pekee atakayekosekana
Aucho anaendelea na 'recovery' baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti wiki iliyopita
Lakini Azam Fc watarajie kukutana na Mburkinabe Stephane Aziz Ki ambaye yuko katika kiwango bora
Ki ndiye kinara wa mabao katika ligi kuu ya NBC akiwa na mabao 13
Kinachoweza kuwatisha zaidi Azam Fc ni rekodi yake kila anapokutana na timu hiyo
Katika misimu miwili Aziz Ki amefunga mabao matano katika michezo dhidi ya Azam Fc
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana, Ki aliyepeleka kilio Chamazi, akifunga mabao yote matatu hat-trik na kuihakikishia Yanga ushindi muhimu wa mabao 3-2
Bila shaka Ki leo ataendeleza rekodi yake nzuri dhidi ya waoka mikate hao