Mabingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) maarufu kombe la FA, Yanga, watakipiga mechi ya 16 bora ya kombe hilo dhidi ya Dodoma Jiji
Mechi hiyo imepangwa kupigwa Aprili 10 kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na TFF, klabu ya Simba itasafiri mkoani Kigoma kuikabili Mashujaa Fc Uwanja wa Lake Tanganyika, Aprili 9
Azam Fc itakuwa nyumbani, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar
Ratiba hiyo ya raundi ya nne ya Kombe la FA inaonyesha kuwa mechi hizo zitaanza Aprili 2 wakati Namungo itakapokuwa nyumbani, Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, Lindi dhidi ya Kagera Sugar
Aprili 3 kwenye Uwanja wa Nyankumbu, Geita kutakuwa na mechi kati ya Geita Gold dhidi ya Rhino Rangers, huku Aprili 4 kukiwa na mchezo kati ya Singida Fountain Gate dhidi ya Tabora United, Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza
Timu ya Coastal Union itakuwa nyumbani, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ikiialika JKT Tanzania, wakati KMC itaikaribisha Dar es Salaam, Uwanja wa Azam Complex, Ihefu FC.