Kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns, uongozi wa Yanga umekuja na kampeni ya kutembelea Matawi yote ya Yanga jijini Dar es salaam kuwahamasisha Wanachama kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa March 30
Meneja wa Habari na Mawasiliano Ali Kamwe jana aliongoza zoezi hilo akitembelea Matawi mawili akianzia Yanga Elites lililopo Dar Free Market na tawi la Yanga Gerezani
Zoezi hilo linaendelea leo katika Matawi mengine ndani ya jiji la Dar es salaam
Jana Yanga ilitangaza viingilio vya mchezo huo ambapo mashabiki 48,000 watapata nafasi ya kushuhudia mchezo huo BURE
Yanga imepania kushinda mchezo dhidi ya Mamelodi, silaha ya kwanza ni kuhakikisha dimba la Mkapa linajaa
ADVERTISE HERE