Tiketi za VIP A zimemalizika! Hii inaonyesha ni kiasi gani Wananchi wameupania mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns ambao utapigwa Jumamosi ijayo, March 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Tiketi ambazo bado ziko katika mauzo ni VIP B na C pekee kwani Mzunguuko na Machungwa ni SOLD out tangu siku ya kwanza baada ya uongozi wa Yanga kuondoa viingilio katika majukwaa hayo ili kuwapa fursa mashabiki waliowengi kujitokeza kuiunga mkono Yanga katika mchezo ambao Wananchi wanahitaji ushindi
ADVERTISE HERE