Jana kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua alikuwa sehemu ya wachezaji wa akiba kikosi cha timu ya Taifa ya Ivory Coast kilichochuana na Benin huko Ufaransa mchezo ukimalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2
Kujumuishwa kwa Pacome katika kikosi licha ya kuwa hakutumika ni ishara kuwa fundi huyo wa mpira yuko fit
Sasa ni uhakika Pacome anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoikabili Mamelodi Sundowns robo fainali CAF CL
Ivory Coast watacheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Uruguay siku ya Jumanne ambapo baada ya mchezo huo Pacome atarejea nchini kuungana na kikosi cha Yanga kuelekea mchezo dhidi ya Mamelodi utakaopigwa Jumamosi ijayo
Nyota wengine wa Yanga ambao walikuwa viwanjani jana katika majukumu ya timu za Taifa ni pamoja na mlinda lango Djigui Diarra aliyeiongoza Mali katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mauritania
Kennedy Musonda alianza katika kikosi cha Zambia kilicholazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Zimbwabwe akitoa assist ya bao la kwanza
Stephane Aziz Ki akiwa na Burkina Faso wakakubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Libya. Mchezo mwingine wa Burkina Faso utapigwa Jumanne, March 26 dhidi ya Niger
Wachezaji Bakari Mwamnyeto na Aboutwalib Mshery wao watakuwa uwanja kesho Jumatatu katika mchezo wa FIFA Series 2024 dhidi ya Mongolia
Hadi kufikia Jumatano, nyota wote wa Yanga walio katika majukumu ya timu za Taifa wanaweza kuwa wamerejea tayari kwa mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns