Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema hatua waliyofikia katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu haikuja kwa bahati, na hawafikirii kama juhudi zao zinapaswa kuishia hapa
Arafat amewataka Wanachama na Mashabiki wa Yanga kuamini wana timu bora ambayo itakwenda kuwapa furaha siku ya Jumamosi katika mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns
"Wananchi dhahabu safi huoshwa kwa moto nasi ni ile dhahabu bora. Ili tuwe na thamani sokoni lazima tupite katika moto mkali"
"Huwezi kuwa bingwa pasipo kumfunga bingwa. Tunaingia katika mchezo huu tukiwa na imani kubwa kwa timu yetu"
"Naiona Yanga ikicheza fainali ya ligi ya mabingwa msimu huu, ni ndoto ya kutisha lakini tupo kwa ajili ya kuandika historia"
"Wananchi wakisema haiwezekani waambieni sisi tutajaa kwa wingi Lupaso. Watakaokuwa nyumbani nao washangilie kwa nguvu zote"
"Weka mkono kifuani amini tunaenda kuandika historia kwani wakati ni sasa kuliko wakati mwingine wowote," sehemu ya maneno ya Arafat