Baada ya kumaliza majukumu yake katika timu ya Taifa ya Ivory Coast, kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua jana jioni alirejea nchini na moja kwa moja kuelekea kambini Avic Town kuungana na wenzake wanaokamilisha maandalizi ya mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa Jumamosi March 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mlinzi wa kulia Yao Kouassi alikuwepo uwanja wa ndege kumpokea rafiki yake huyo akiwa sambamba na Aubin Kramo anayeitumikia klabu ya Simba
Yao anaweza kuwa 'surprise' siku ya Jumamosi kwa kuwakabili Mamelodi Sundowns kwani taarifa za ndani zimedokeza kuwa afya yake imeimarika
Leo Yanga itakuwa na nafasi ya kufanya mazoezi katika uwanja wa Benjamin Mkapa mapema kabla ya kuzipisha klabu za Mamelodi na Al Ahly
Mamelodi watalazimika kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja huo leo kwani kesho kutakuwa na mchezo kati ya Simba dhidi ya Al Ahly