Shamrashamra na hamasa kuelekea mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns, zinahitimishwa leo Tandika Sokoni, Temeke jijini Dar es salaam
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe pamoja na timu nzima ya hamasa watakuwepo Tandika kuwakaribisha Wananchi uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumamosi
Kamwe amesema wanahitimisha zoezi la hamasa leo ili siku ya kesho kuwapa nafasi watani zao Simba ambao watachuana na Al Ahly katika mchezo wa kwanza wa robo fainali
Mechi hiyo pamoja na ile ya Jumamosi zitapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa saa 3 usiku
ADVERTISE HERE