Mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga leo watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Mamelodi Sundowns katika mchezo wa mkondo wa kwa robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Matumaini ya Watanzania yamebaki mikononi mwa Yanga baada ya watani zao Simba kuangukia pua hapo jana kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Al Ahly
Mechi ya Yanga dhidi ya Mamelodi ndio iliyozungumzwa zaidi na pengine inatizamwa kuwa mechi bora zaidi katika hatua ya robo fainali
Aina ya uchezaji wa timu hizo unafanana, lakini rekodi ya Yanga katika uwanja wa Benjamin Mkapa inawafanya wengi waamini leo wanaweza kufanya lisilotarajiwa na wachambuzi wengi wa soka nchini ambao wamekuwa wakiipa Yanga nafasi ndogo ya kushinda
Lakini pia hii ni mechi ambayo Yanga inaweza kuitumia kuinonyesha Afrika daraja walilopo. Inaaminika Mamelodi Sundowns ndio klabu bora barani Afrika kwa sasa
Kama Yanga inaweza kupata ushindi dhidi ya Mamelodi maana yake watadhihirisha wamefika katika daraja la timu bora barani Afrika
Ni wazi haitakuwa mechi nyepesi, Mamelodi wamejipambanua kwa kuwa hatari zaidi wanapocheza ugenini pengine kuliko nyumbani
Wanakutana na Yanga ambayo pia ina rekodi nzuri inapocheza nyumbani ikifunga mabao nane nyumbani na bao moja tu ugenin katika hatua ya makundi
Mchezo huo unatarajiwa kushuhudiwa na maelfu ya mashabiki kwani takribani watu 48,000 wataingia bure majukwaa ya Mzunguuko na Machungwa
Kila la kheri Yanga, kila la kheri mabingwa wa nchi...!