Mkataba mpya unamsubiri Gamondi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Apr 2024
Mkataba mpya unamsubiri Gamondi Yanga

Baada ya kuirejesha heshima ya Yanga katika michuano ya ligi ya mabingwa, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amebaki na kazi moja tu, kutetea mataji ya ligi kuu na kombe la Shirikisho la CRDB

Kocha huyo raia wa Argentina amevuka malengo ya Yanga katika ligi ya mabingwa baada ya kuipeleka robo fainali na kushuhudia ikitolewa kwa 'figisu' dhidi ya Mamelodi Sundowns ambapo Afrika na dunia ilishuhudia mbeleko ya chuma ikitumika kuibeba Sundowns baada ya Yanga kunyimwa bao halali lililofungwa na Stephane Aziz Ki katika dakika ya 57

Wakati akitua Yanga, Gamondi alisaini mkataba wa mwaka mmoja uliokuwa na kipengele cha kuongeza mwaka wa pili mwishoni mwa msimu

Kwa kile ambacho ameifanyia Yanga mpaka sasa, bila shaka uongozi wa Yanga chini ya Rais Injinia Hersi Said utamuongeza mkataba

Jukumu lake ni kuhakikisha Yanga inatetea taji lake la ligi kuu na taji la FA ambayo Wananchi wanayashikilia kwa misimu miwili mfululizo

Kesho Yanga itashuka uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma kumenyana na Dodoma Jiji katika mchezo wa kuwania tiketi ya kutinga robo fainali kombe la FA

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’