Tuko tayari kuikabili Singida FG - Gamondi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Apr 2024
Tuko tayari kuikabili Singida FG - Gamondi

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida FG utakaopigwa kesho Jumapili katika uwanja wa CCM Kirumba

Licha ya kikosi chake kucheza mechi siku mbili zilizopita, Gamondi amesema wamefanya maandalizi kwa kuzingatia mhitaji ya mchezo huo

Kuhusu hali za wachezaji majeruhi Gamondi amesema baada ya mazoezi ya mwisho leo atafahamu wachezaji ambao watakuwa tayari kutumika hapo kesho

"Leo jioni tutafanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Singida Big Stars na mazoezi yetu ya leo yatatupa mwelekeo wa Wachezaji gani tutaweza kuwatumia kwenye mchezo wa kesho"

"Falsafa ya kwanza ya Young Africans SC ni timu na siyo Mchezaji mmoja mmoja, wenyewe mmekuwa mashahidi michezo yetu iliyopita tulikuwa na majeruhi lakini kila Mchezaji aliyepata nafasi ya kucheza amefanya kazi yake vizuri"

"Napenda pia kuwapongeza Mashabiki wetu kwa kazi nzuri wanayoifanya kila mahali tunapokwenda kucheza na nilishangaa Mashabiki wetu hapa Mwanza kwenye mchezo tuliocheza hapa dhidi ya Geita, walikuwa wanashangilia kwa nguvu muda wote wa mchezo ilikuwa ni kama niko Amerika Kusini na najua kesho watakuja kwa wingi kutupa sapoti"

"Maandalizi ni ya kawaida kwa sababu tumetoka kucheza juzi na tunajua mchezo wa kesho utakuwa mgumu lakini tumejiandaa kuhakikisha tunafanya vizuri," alisema Gamondi

Kikosi cha Yanga kilitua Mwanza jana usiku na jioni ya lo watajifua katika uwanja wa CCM Kirumba utakaotumika hapo kesho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
2h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
21h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’