Yanga inahitaji ushindi dhidi ya Singida FG hapo kesho ili kuendelea kuukaribia ubingwa wa 30 ligi kuu ya NBC
Baada ya Simba kulazimishwa sare dhidi ya Ihefu Fc maana yake ni kuwa sasa iko nyuma kwa tofauti ya alama sita dhidi ya Yanga huku timu zote zikiwa zimeshuka dimbani mara 20
Azam Fc inayoshika nafasi ya pili iko nyuma ya Yanga kwa tofauti ya alama tano huku ikiwa imecheza mechi moja zaidi
Kama Yanga itapata ushindi dhidi ya Singida FG, itaongeza gap la pointi dhidi ya Azam Fc kuwa nane na Simba kuwa tisa
Wananchi wanatamba kileleni na alama 52, Azam Fc nafasi ya pili alama 47 na Simba nafasi ya tatu alama 46
ADVERTISE HERE