Mapema leo, uongozi wa Yanga chini ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga Makaga na Alexander Ngai, Mtendaji Mkuu Andre Mtine, Mkurugenzi wa Masoko na Wanachama Ibrahim Samweli pamoja na Meneja wa Habari na Mawasiliano Ally Kamwe walikaa kikao na Viongozi wa Matawi ya Wanachama Kanda ya Ziwa
Kikao hicho kilikuwa na lengo la kuhamasisha ulipaji wa Ada kwa Wanachama na Mashabiki pamoja na kuzungumzia mambo mbalimbali ya maendeleo ya klabu ya Yanga
Mkutano huo ulihudhuriwa na Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda, Mkuu wa Mkoa Mstaafu Mhe. Said Meck Sadiki pamoja na wadhamini kampuni ya SportPesa, NMB Bank, CRDB Bank na Hospitali ya Aga Khan






ADVERTISE HERE