Ukimuangalia Jonas Mkude 'Nungunungu' ni kama amezaliwa upya katika kikosi cha Yanga
Tangu arejeshwe kikosini katika mchezo wa ligi ya mabingwa, CAF CL dhidi ya Mamelodi Sundowns, Mkude sasa amekuwa ni mchezaji tofauti
Ameendelea kuwa muhimiri katika eneo la kiungo jana kocha Miguel Gamondi akimuanzisha na Khalid Aucho katika mchezo dhidi ya Singida FG huku Mudathir Yahya akianzia benchi
Upande wa kulia muangalia Gift Fred anavyocheza! Hii ni 'sapraizi' nyingine kwa Kocha Miguel Gamondi
Gamondi ni kama alifanya majaribio kwa kumtumia Gift safu ya ulinzi upande wa kulia katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Dodoma Jiji
Baada ya kuonyesha kiwango bora katika mchezo huo, jana katika mchezo dhidi ya Singida FG akamtumia tena katika nafasi hiyo na akan'gara
Fred ameonekana kuwa bora zaidi katika ulinzi na mara nyingi sio rahisi kupitika katika 1 vs 1
Muangalie Clement Mzize alivyocheza mechi mbili zilizopita. Alibeba tuzo ya mchezaji bora wa mechi ya FA dhidi ya Dodoma Jiji na jana katika mchezo dhidi ya Singida FG alistahili kubeba tuzo hiyo kama ingekuwa ikitolewa. Alitoa assist mbili katika mchezo ambao Yanga ilishinda mabao 3-0
Joseph Guede jana akawaonyesha Wananchi uwezo wake halisi akifunga mabao mawili katika ushindi dhidi ya Singida FG
Kelele zilishaanza kuwa nyingi huko mitaani lakini baada ya mabao yake bora hapo jana, amerejesha utulivu
Guede tayari ameifungia Yanga mabao manne katika mashindano yote tangu alipotua kwa Wananchi usajili wa dirisha
Katika mechi mbili zilizopita Wananchi hawakumuona Kennedy Musonda ambaye alin'gara katika mechi za ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns
Musonda alipata majeraha madogo katika mchezo wa pili dhidi ya Sundowns na Gamondi kuamua kumpumzisha ili apone vyema
Ikumbukwe pia katika mechi nne zilizopita sio Yao Kouassi wala Pacome Zouzoua aliyeonekana katika kikosi cha Yanga
Yao alikuwepo Mwanza lakini Gamondi aliamua kutomtumia akilenga kumuandaa kwa ajili ya mechi dhidi ya Simba
Ni wazi hata Pacome atakuwa tayari katika mchezo huo lakini hata akikosekana, kwa ubora wa kikosi chao Wananchi hawatakuwa na maswali
Wachezaji kama Salum Abubakar 'Sure Boy' na Augustine Okrah waling'ara katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji lakini Gamondi jana akawapumzisha
Aziz Ki ameendelea kuwa injini ya mabao msimu huu akipachika mabao 14 na kutoa assist 7 katika ligi kuu ya NBC
Muangalia Maxi Nzengeli sasa amerejea katika ubora wake baada ya kupitia kipindi kigumu hasa baada ya ule mchezo wa 5G dhidi ya Simba
Diarra, Job, Bacca, Mwamnyeto, Lomalisa hawa wameendelea kuwa nguzo imara katika safu ya ulinzi wakiifanya Yanga kuwa timu iliyofungwa mabao machache zaidi katika ligi kuu ya NBC
Itoshe kusema kwa sasa Yanga iko imara kama timu, kwa hakika hiyo April 20 Simba watakuwa na kazi kubwa mbele ya vijana wa Gamondi