Droo ya hatua ya robo fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB Bank imefanyika leo ambapo mabingwa watetezi wa michuano hiyo Yanga watachuana na Tabora United mchezo ukitarajiwa kupigwa jijini Dar es salaam
Mechi za robo fainali zitapigwa kati ya Mei 2-4 mwaka huu (2024)
Mechi nyingine za robo fainali Azam Fc watachuana na Namungo Fc wakati Coastal Union wakichuana na Geita Gold
Mchezo mwingine ni kati ya Ihefu Fc dhidi ya Mashujaa Fc
Katika hatua ya nusu fanali, mshindi wa Mchezo kati ya Azam Fc dhidi ya Namungo atakutana na Mshindi wa Mchezo kati ya Coastal Union dhidi ya Geita Gold
Aidha mshindi wa Mchezo wa Yanga dhidi ya Tabora United atakutana na Mshindi wa Mchezo wa Ihefu Sc dhidi ya Mashujaa Fc katika nusu fainali
ADVERTISE HERE