Wakati tetesi kuhusu klabu ya Azam Fc kutuma ofa Yanga kumtaka mshambuliaji Clement Mzize, mabingwa hao wa Tanzania Bara tayari wamekamilisha mazungumzo kwa ajili ya kumuongeza mkataba
Mzize amekuwa katika kiwango bora msimu akiwa mmoja wa wanaoaminiwa katika kikosi cha kocha Miguel Gamondi
Yanga tayari imekamilisha mazungumzo na mchezaji huyo ambapo anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu ambapo maslahi yake yameboreshwa zaidi
Jana msemaji wa Azam Fc Hashim Ibwe alitamba kuwa wamewasilisha ofa nono kwa Mzize pamoja na mchezaji mwingine mwenye wasifu mkubwa katika kikosi cha Yanga
Ni kama ile vita ya usajili ambayo Azam Fc waliianzisha msimu uliopita dhidi ya Yanga bado haijapoa
Baada ya kuwasajili Feisal Salum, Djuma Shabani na Yannick Bangala, msimu huu Azam Fc tayari wamempoteza Prince Dube aliyejiondoa kikosini huku akifungua madai Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF kupinga madai ya Azam Fc kuwa aliongeza mkataba wa miaka miwili juu ya mkataba wake wa awali
Kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa leo Dube akisisitiza kuwa mkataba wake na Azam Fc unamalizika mwishoni mwa msimu huu
Tetesi ni kuwa Mwana wa mfalme atakuwa mchezaji wa kwanza kutambulishwa na Wananchi katika usajili wa kuelekea msimu ujao